Exodus 40:21-32

21 aKisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza.

22 bMose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 23 cna kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

24 dAkaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu 25 ena kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

26 fMose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia 27 gna kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Bwana alivyomwagiza. 28 hKisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu.

29 iMose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Bwana alivyomwagiza.

30 jAkaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, 31 kNaye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. 32 lWakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Copyright information for SwhNEN